RITA 49.
Alipomaliza kunionyesha zile kamera za alisimama na kuelekea sebuleni akaniacha mdomo wazi.
"Ama kweli dunia kuna mambo. Kumbe usilolijua ni usiku wa giza?" Nilibaki nikijuliza maswali.
Hatma yangu ya kutaka kutoroka na kuelekea pasipojulikana iligonga mwamba, singeweza tena kutoka siku ile Kama nilivyokuwa nimepanga.
Nilijaribu kuelekeza fikra zangu zote kwa televisheni lakini nikashindwa, nikagaragara kochini Kama kuku aliyetaka kutaga mayai.
Niliuchukua mkongojo wangu na kurudi kwenye chumba Cha kulala, nikalala kifudifudi huku bado nikiwaza ulimwengu na malimwengu yake.
Nilipokuwa nimezama kwenye mawazo mlango wa chumba nilichokuwepo ulifunguliwa ghafla.
Bahati alikuwa amesimama mlangoni huku mkono wake wa kushoto kashika nyonga na kutia kidole cha kati Cha mkono wa kulia kinywani.
Bahati alikuwa na Bahati ya kuzaliwa.
Ile kanchiri nyeupe aloivaa iliinuliwa na maziwa yake makubwa kiasi kisha kitovu chake kikaonekana ambacho kilikuwa na kashimo.
Tumbo lake halikuwa kubwa, lilipendeza. Kisha kiuno chake kilikuwa na kilima huku makalio yake yakiwa makubwa kiasi. Alikuwa na umbo la nambari nane.
"Mbona unaniangalia hivyo? Unataka kuniona vizuri ee?" Bahati aligeuka, akatikiza tako lake kana kwamba alitaka kunieleza alichokuwa amemiliki.
"Mbona umetoa nguo? Umeamua kutembea uchi?" Nilimwuuliza.
"Kuna joto." Alinijibu, akaukomelea mlango kwa kufuli.
" Unataka kufanya nini?" Nilishtuka, nikaketi kitandani.
"Kwani unaniogopa? Mimi si mnyama uniogope." Alikenua, akatembea jinsi wafanyavyo wanadada wanaofanya katika shindano la miss Kenya.
"Sijasema wewe ni mnyama lakini vitendo vyako ni unyama." Nilimjibu huku nikiwa tayari kusimama.
" Unaenda wapi?" Aliniwahi kabla ya kusimama, akaniketisha kwa kitanda.
"Kama nilivyokwambia hapo awali ni kuwa nimeoa, sitaki kukukosea heshima." Nilimjibu. Kimya kilitawala huku bado akiwa amenishika mikono.
"Mke wako ako hapa? Hebu wacha upuzi." Alinikaripia.
"Hayuko lakini nampa heshima zake, heshima si utumwa. " Nilimjibu.
" Amefunga kufuli ndio nisiibe eeeh! Maneeno hayo." Alicheka kwa sauti, akanitazama kisha akacheka tena.
" Hata kama umeoa au kuolewa hiyo si haja yangu, nachotaka ni..." Alitazama uume wangu.
" Kama nilivyokwambia, sitaki nikudanganye. Penzi langu kwako halipo, utajikosea kwa kujiumiza bure. " Nilimjibu.
" Nipo radhi kujiumiza. Mtoto akililia wembe si umpe tu nawe?"
" Hapana si... "
" Hapana nini?" Bahati alitoa makucha. yake tayari kupasua windo lake.
Alinitazama kwa hasira, moyo wake ukaanza kupiga kwa kasi hadi nikahisi mapigo yake.
"Unaniumiza Jasiri! Kwani waniona Malaya? Nachukia wanaume lakini nimekupenda wewe. Kusema kweli sijawahi fanya mapenzi na wanaume;nawachukia." Bahati alianza kudondokwa na machozi.
" Basi nipe busu." Aliinuka na kuketi kwa mapaja yangu."
" Auuch! Unaniumiza Bahati."
" I'm sorry." Aliniomba radhi.
Mtego wa Bahati ulikuwa umenasa windo. Nilijaribu kupiga hesabu ya kujinasua kutoka kwa ule mtego nikashindwa.
Damu yangu pia ilikuwa imeanza kuchemka nikafunga macho na kumwomba Mungu aniepushie karaha.
Nilitaka kumsukuma Bahati kisha niondoke ila nikakumbuka hiyo ilikuwa kazi bure. Kwanza, Bahati alikuwa bonge la Jike lililokuwa limefungasha si haba. Hivyo hata ningemsukuma ingekuwa Kama kumsumuma ndovu asikulalie.
Pili, mlango ulikuwa umekomelewa kwa kufuli.
Nilipokuwa nimefunga macho, midomo ya Bahati ilikutana na yangu, akanibusu hadi mwili wangu ukasisimka. Bahati alikuwa daktari wa kubusu.
Alinirusha kitandani, "auchh! Unaniumiza jamani na sijapona." Nilalamika huku nikiwa nimelala chali.
" I'm sorry, " aliongea kwa sauti iliokuwa imelegea.
Alivua ile kanchiri, maziwa yake yakabaki yakiwa tisti kana kwamba yalitaka kutoboa macho yangu.
Bahati alikuwa ameamua kufuata vitendo bila kuongea.
Alikuwa simbamarara ambaye alikuwa tayari kurarua windo lake. Alishika shati langu na kurarua vufunguu ungedhani alikuwa anataka vita.
"Ngrrr! ngrrrrr!" Kengele ya mlango ililia.
"Kuna mgeni jamani, enda ukamwone." Nilimjibu kwa haraka.
"Bahati alisonya, akainuka shingo upande na kuvaa kanchiri yake.
Nilibaki na mchanganyiko wa mawazo; furaha na huzuni. Nilifurahi kwa kuwa sikufanya mapenzi na Bahati, nikahuzunika kwa sababu msichana mrembo alikuwa ameniponyoka.
Nilisimama polepole kwa mkongojo wangu na kuelekea sefuni,nikachukua long'i pamoja na shati nikavaa. Nikarudi na kuketi kitandani.
"Bob,... Bob!... Bob!" Bahati aliniita.
"Nan...naam.'' Niliitika baada ya kukumbuka kuwa Bob ndilo lililokuwa jina langu jipya mtaani.
"Njoo umsalimie mgeni." Bahati aliongea kutoka sebuleni.
"Huyu atakuwa mgeni yupi? Au Bahati amenisaliti?" Moyo wangu ulienda mbio. Niliogopa maana tangu nijipate kwa Bahati sikuwahi mwona mtu yeyote akiingia humu.
Nilitaka kumwuuliza kuhusu wazazi wake lakini haikuwa vyema; nilingoja tu hadi pale atakaponielezea maana sikutaka kuonekana mtu asiye na adabu.
Nilitembea polepole hadi sebuleni, nikamwona Bahati ambaye alikuwa amevaa dera. Mama mwenye miaka hamsini hivi alikuwa ameketi karibu na mlango wa kuingia sebuleni.
Ungemtazama vizuri alikuwa na mshabaha na Bahati. Pia sura yake ilikuwa kwenye picha zilizokuwa zimetumdikwa ukutani.
"Huyu ndiye Bob niliyekuambia mama." Bahati alikuja na kukati kando yangu.
"Shikamoo mama," nilimwamkua.
"Marahaba mwanangu. Pole kwa kuhusika katika ajali mwanangu."
"Nishapoa mama." Nilimjibu.
" Mimi naitwa Zena, mamake Bahati." Alijitambulisha.
"Nami naitwa Ja..."
"Aumhhhh" Bahati alijitia kikohozi.
"Naitwa Bob mama." Nilikumbuka jina langu la pili.
"Ooh mwanangu alikuwa amenieleza kukuhusu. Hakosi kuniambia jinsi ulivyo mpole na anavyokupenda. Nilitaka kuja hata hospitalini kukuona lakini sikupata nafasi ya kufika Nairobi ulipokuwa umelazwa na kurudi kutokana na kazi. Natumai hutamvunja mwanangu moyo. Huyu ndiye kinda wa pekee. Mboni ya jicho langu." Bi. Zena aliongea kwa matumaini makubwa.
" Katu siwezi." Nilimjibu ingawa moyoni nilikuwa na maswali mengi.
Sikujua mbona Bahati alimdanganya mamake mzazi kuwa mimi nilikuwa mchumba wake. Halafu kisa Cha kumfanya mamake aamini kuwa nilikuwa nimelazwa hospital ya Nairobi kilikuwa ndoto. Nilitaka kucheka lakini nikajizuia, nikaangalia chini.
"Nilipopata mimba ya Bahati babake aliniringa na kukataa kuwa mimba haikuwa yake. Sikujua mbona alinidanganya kuwa angenioa pindi ningepata mimba. Aliniacha nikiwa sina chochote, akaelekea Marekani hadi sasa.
Sijui mbona nimeamua kukueleza hili lakini imebidi nikueleze maana ninajua kuwa wewe ni mtu mzuri. Utamlea mwanangu." Alikimya baada ya kumaliza kauli yake huku machozi yakimdondoka.
"Pole kwa yaliyokufika mama, dunia rangi rangile." Nilimjibu.
"Sawa mwanangu, Mimi naomba kuwaacha." Zena alitaka kuondoka.
" Hapana mama, ngoja tukapike." Bahati alimwomba mamake.
" Ndio mama, mbona haraka?" Nilidakia.
"Sawa basi" alikubali.
Mama na mwanawe wakaelekea jikoni na kuniacha sebuleni.
TUTAIENDELEZA
Comments